Madaktari hao wakiwa na baadhi ya Mabango.
leo mchana kuliibuka na maandamano ya watu waliojitambulisha kuwa wanadimokrasia, na baadhi yao madaktari waliandamana kuishinikiza serikali isikilize kilio cha madaktari.
Waandamanaji hao wakiwa na mabango waliziba barabara ya Ally Hassan Mwinyi maeneo ya Salenda na kusababisha usumbufu na foreni kubwa ya magari katika barabara hiyo.
Hospital ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, juzi (Jumanne) ilitawaliwa na vilio vya wagonjwa baada ya madaktari bingwa nao kugoma kutibu.
Vilio hivyo vilivyoshuhudiwa na waandishi wetu vilikuwa ni vya wagonjwa ambao walidai kukosa tiba licha ya kuwa katika hali mbaya kiafya katika hospitali hiyo kufuatia mgomo wa madaktari hao bingwa.
Azimio la mgomo huo lilifikiwa katika kikao cha dharura kilichoitishwa na jopo la madaktari bingwa wakiongozwa na Dk. James Rwehabura ambaye ni daktari bingwa wa Kitengo cha Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu.
“Nina siku tatu hapa sijapata tiba yoyote,” alilalamika mgonjwa mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Saidi Ally. Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano(tunayo nakala yake) imesema mpaka juzi kulikuwa na wagonjwa 811 hospitalini hapo, lakini waandishi wetu walishuhudia wengine wakigeuza na kurudi walipotoka.
Wakati ofisi hiyo ikisema wagonjwa watatibiwa na madaktari ambao ni wakuu wa idara, wagonjwa wamekanusha kuwaona vigogo hao wakitoa tiba. Waandishi wetu walikataliwa katakata kuingia katika wodi namba 17 na 18 katika Taasisi ya Mifupa (Moi) hospitalini hapo ambako kunadaiwa hali ni mbaya na wagonjwa wanaoza kutokana na majeraha waliyopata katika ajali.
Madaktari hao bingwa wamegoma kufuatia kile walichodai kuwa ni kuzidiwa na kazi na kuwa na mazingira magumu ya kazi baada ya madaktari wenzao waliokuwa wakiwasaidia kugoma.
BFTZ SHARING IS CARING
No comments:
Post a Comment