The path to success

Wednesday, 1 February 2012

ASKARI JWTZ WALIPILIWA NA MABOMU GONGO LA MBOTO la mboto hoi




                     moja ya nyumba iliyobomolewa na mabomu hayo

HALI za askari wa  Jeshi la Wananchi wa Tanzania ‘JWTZ’  katika Kambi ya 511 jijini Dar es Salaam ni mbaya kutokana na ucheleweshwaji wa malipo ya fidia za  nyumba walizokuwa wakiishi ambazo zililipuliwa na mabomu mwaka jana.
Askari hao wapatao 85, wakizungumza na waandishi wetu kwa nyakati tofauti  wamedai kwamba  tangu walipokumbwa na masaibu hayo Februari 16, mwaka jana wanaishi kwa tabu.
Wapiganaji hao wakizungumza kwa uchungu kwa sharti la kutoandikwa majina yao kwa sababu za kimaadili, wamedai kwamba wanalalia mikeka na kukaa sakafuni na familia zao licha ya makao makuu ya jeshi hilo kufanya tathmini ya vitu vyao vilivyoharibika na kuahidiwa fidia.
“Wizara iliunda tume iliyoongozwa na Kanali Temu kutoka Kikosi cha 603 Air Wing, kuja kufanya tathmini ni hasara kiasi gani tumepata, zoezi hilo lilifanyika Mei mwaka jana  lakini mpaka sasa hatujui kinachoendelea,” alisema mpiganaji moja.
Mwingine alidai kwamba  walifarijika sana walipoona viongozi wao wamechukua hatua hiyo ya tathmini ya hasara waliyopata na walikuwa na imani kwamba wangelipwa fedha mapema ili waweze kununua samani nyingine.
Walisema kwamba  wanashangaa kuona raia waliopata matatizo ya nyumba kubomolewa wamelipwa lakini wao hawajui  kinachoendelea.
Wanajeshi hao waliongeza,   baadhi yao  walipoteza vitu vingi kutokana na mlipuko hiyo yakiwemo magari ambapo hivi sasa wamebaki maskini kana kwamba ndiyo wanaanza maisha.
 “Wengine wamekaribia kustaafu na hali ikiendelea hivi, watatoka maskini, yaani mikono mitupu ingawa walikuwa na maisha mazuri kabla ya milipuko kutokea,” alisema mmoja wa askari hao.
Hata hivyo, wanajeshi hao wamemshukuru  Waziri wa Ulinzi  na Jeshi la Kujenga Taifa,  Dk. Hussen Mwinyi  kwa kuwafariji baada ya kutokea milipuko hiyo.
Mmoja wa askari hao alisema, waziri huyo alipofika kujionea athari za mabomu, aliwahamasisha  watu  ambao waliwachangia fedha, chakula na nguo  ambapo jumla ya shilingi milioni 56 zilipatikana na kila askari alipata mgawo wa shilingi 600,000 ambazo ziliwasaidia kununua chakula kwa kipindi hicho.
 “Tangu waziri aache kututembelea  hakuna msaada ambao tunafikishiwa  licha  ya kupewa nyumba ambazo tuliingia bila kuwa na kitu  chochote zaidi ya vyombo vya kupikia tulivyosaidiwa na majirani,” alisema askari mwingine.
 Walidai kwamba  wanashangaa kwa nini  wasilipwe  wakati  Waziri Mwinyi aliwatangazia  kwamba wangelipwa mapema lakini sasa wanapigwa chenga.
Askari hao wamemuomba Waziri Mwinyi awasaidie waweze kulipwa fedha hizo ili waondokane na maisha ya dhiki.
Nao askari vijana wasiooa ambao walikuwa wakiishi katika hanga lililolipuliwa na mabomu, walidai kuwa hawajapata  kitu  chochote na  kwamba  sasa  wanaishi katika mahema ambayo huwapa mateso wakati wa jua kwa sababu ya joto.
“Wakati wa mvua huwa tunanyeshewa kutokana na mahema kuchakaa, hivyo kusababisha mbu kuingia na kutudhuru,” alilalamika mmoja wa askari hao ambaye alidai wanalala  nane katika hema moja.
Mmoja wa waandishi wetu alipowasiliana  na Msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Luteni Kanali Mgawe alisema, kwa sasa yupo likizo.
Mwandishi wetu alipozungumza na msaidizi wa Mgawe aliyejitambulisha kwa jina la Meja Komba, alisema kuwa suala hilo linashughulikiwa ndani ya jeshi hilo, litakapokamilika litawasilishwa ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa.
Waziri Mwinyi alipozungumza na Uwazi alisema: “Nafuatilia suala hilo, nashindwa kuelewa kwa nini fidia hazijalipwa, nafuatilia kujua zilipokwama.”
    Source:global pub
BFTZ SHARING IS CARING
    lisher

No comments:

Post a Comment