The path to success

Sunday 5 February 2012

WAKATI MWINGINE UMASKINI WETU NI WAKUJITAKIA SISI WENYEWE NA NIJIHUDI ZETU ZITAKAZOTUFANYA TUTOKOMEZE UMASKINI KATIKA MAISHA YETU, KUKIMBIA TATIZO SIO KUTATUA TATIZO


KAMA BABA YAKO ALIKUTELEKEZA BAADAE UKAWA MAMBO SAFI AKARUDI KUOMBA RADHI, JE UTAMSAMEHE?? AU UTAMPOTEZEA??




NAKALA HII NIMEITOA KA LADY JAY DEE NANIKAONA SIMBAYA KUSHARE NA NYIE HAYA ENDELEA ....

Madai kutoka kwa mzee Samuel Manyapye pichani juu

Ni kuwa miaka kadhaa iliopita aikuwa na girlfriend wake ambae hivi sasa ni marehemu Bi Mahlodi Malema wakafanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume JULIUS MALEMA

Ambae ni mwanasiasa mkubwa tu na mambo yake kiuchumi sio mabaya.

Mzee kwa madai yake, alimtelekeza girlfriend akiwa na mtoto mdogo

Akazama kwenye penzi la mwanamke mwingine ambae kwa sasa wana watoto 7 pamoja.

Ninapoongelea kuwatelekeza sio ile kuwa labda hata mara moja moja anapita kumuona mtoto la hasha!!!

Telekeza hii ni ya kupotea kabisa, kukata mawasiliano na kutojulikana yuko wapi

Na hakuwahi kutuma matumizi ya mtoto, wala kujua mtoto anasomaje wala kula nini, kwa maana hiyo mtoto mpaka anakua mkubwa hamjui baba ake ni nani

Saa zingine wamama wanapewaga lawama kuwa wanawapotosha watoto wawachukie baba zao, lakini kwa ishu kama hii ambayo mzee mwenyewe anakiri kuwa alikimbia, inakuwaje?

Maisha ya huyu babu ni ya kimaskini kabisa na anafanya shughuli za kuokota vyuma vilivyotumika kwenda kuviuza ili aweze kulisha familia hiyo ya watu 9

Hii ni sawa na kuruka mkojo kukanyaga mavi, maana alikimbia mtoto mmoja ambae sasa hivi ndio angeweza kumsaidia.

Akakimbilia kwenda kuzaa watoto 7 ambao hivi sana ni vigumu sana hata kuwapatia elimu kwakuwa kipato chake kwa siku akiuza hayo machuma anayookota ni Rand 15 tena hapo ni kama biashara ikichanganya

Ni wastani wa kama Rand 140 kwa mwezi anayopata mzee Samweli ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania kama 30,000/= au pungufu
Watoto wengine anasaidiwa kulea na ndugu kutokana na kibanda anachoishi kuwa hakijitoshelezi kuwahifadhi wote kama familia.

Sasa hivi anarudi na kutaka wapatanishwe na mwanae ambae alimkimbia akiwa mdogo pamoja na mama yake, ila pia hajui aanzie wapi.

sa wanamuelemea.


Bwana Julius Malema katika interview yake moja wapo alinukuliwa akisema

Hajawahi kukutana na baba yake mzazi na wala hajawahi kuwa na baba katika maisha yake

Na kuwa alilelewa na mama na bibi yake mzaa mama tu

Na hajui kitu kingine zaidi ya hao watu wawili

Na kwanini ahitaji baba kwa muda huu ambapo ameshakuwa mtu mzima?


Wengine wanaamini ni game tu kumchafua Julius Malema kisiasa

Wakati mzee akisisitiza yeye ndio baba mzazi

Na yuko tayari kumuomba mwanae msamaha

Je! kama kweli ni baba yake anataka kumuomba msamaha kwakuwa amejuta?

Anahitaji kuwa karibu ili apewe msaada yeye na familia yake iliochoka?

Kama ana huo moyo na mapenzi na kujali kwa mtoto wake

Alikuwa wapi kujitokeza mpaka mtoto amepata umaarufu ndio aje aseme?

Jibu wanalo wao?

Lakini ingekuwa wewe ni Julius Malema na huyo ni baba yako kweli, ungemsamehe?


Mnaokimbia watoto kazi kwenu, unamkimbia mara anakuja kuwa Rais baadae unabakia unajiuma uma sasa.



BFTZ SHARING IS CARING

1 comment:

  1. Anonymous2:07 pm

    nataka kujua kisa cha huyo mama kukimbiwa,wanawake wakati mwingine mnajitakiaga wenyewe!!huwa mnatusema sana lakini mnajisahau ninyi wenyenyewe

    ReplyDelete